Miche zaidi ya 1,000+ ya pandwa kuadhimisha siku ya Misitu Duniani

Miti 1,000+ Yapandwa Kitaifa Kuadhimisha Siku ya Misitu Duniani 2023

Green Awareness Club Tanzania | 21 Machi 2023

Shule 7 • Mikoa 7 • Uelimishaji wa Uhifadhi wa Misitu

Kutokana na Siku ya Misitu Duniani (21.03.2023), Green Awareness Club Tanzania iliendesha kampeni ya kitaifa ya upandaji miti katika shule mbalimbali.

Miche zaidi ya 1,000 ilipandwa katika shule 7 zilizopo mikoa 7 tofauti, sambamba na utoaji wa elimu kuhusu utunzaji wa misitu.

Matokeo ya Kampeni

  • 0 miche imepandwa
  • Shule 7 zimefikiwa
  • Mikoa 7 imehusishwa katika kampeni
  • Uelimishaji wa uhifadhi wa misitu umetolewa kwa wanafunzi

Aidha, Mwenyekiti Taifa wa Green Awareness Club ametoa shukrani kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Chuo cha Misitu Olmotonyi (FTI), halmashauri, na vyombo vya habari kwa ushirikiano.


Matukio kwa Mikoa

DAR ES SALAAM

Shule ya Sekondari Mabibo na Shule ya Msingi Makuburi • miche 150

PWANI

Shule ya Sekondari Mwinyi • miche 100

ARUSHA

Shule ya Msingi Ngorbob – Kisongo • miche 120

KILIMANJARO

Shule ya Msingi Kivulini, Wilaya ya Mwanga • miche 150

GEITA

Shule ya Msingi Ibondo, Wilaya ya Chato • miche 300

DODOMA

Shule ya Msingi NG'ONG'ONA • miche 150

MBEYA

Shule ya Msingi Pambogo • miche 150

Shiriki Nasi Kulinda Misitu Yetu

Jiunge na Green Awareness Club katika kampeni za upandaji miti na uelimishaji wa mazingira ili kuhakikisha Tanzania inabaki kijani.

Jiunge Nasi

#SikuYaMisituDuniani #TreePlanting #GreenAwarenessClub #TanzaniaYaKijani