Usafishaji wa fukwe Kidimbwi beach ( Beach cleanup)
Leo Tarehe 27.08.2022 Green Awareness Club tulishiriki zoezi la kufanya usafi kwenye ufukwe wa Kidimbwi beach area , Indian ocean tukishirikiana na Environmental conservation community of Tanzania ECCT , Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Godwin Gongwe, ambaye amekuwa akihamasisha jamii na wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kushiriki zoezi la usafi Kila mwisho wa mwezi.
![]() |
Mheshimiwa Godwin Gongwe, akishiriki zoezi la usafi. |
![]() |
Wananchi mbalimbali walio jitokeza. |
![]() |
Kutoka Kushoto: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni MHE. Godwin Gongwe na Mwenyekiti wa Green Awareness Club Ndugu. Ibrahim Sinsakala. |